SWAHILI: Wakati wa ukosefu wa ngano nchi nzima Kenya, Ustadh Mau hakuweza kuendelea kufanya kazi dukani kwake la mkate na ndio maana kwa muda alianza kushughulika sokoni kama muuzaji wa nyama. Ustadh alikuwa na miaka 28 takriban kwenye picha.
ENGLISH: During the caresty of wheat in the whole country of Kenya, Ustadh Mau could not work at his bakery and this is why he started for a while to work at the market as seller of meat. Ustadh Mau was around 28 years old.
SWAHILI: Ustadh Mau anapokea zawadi kutoka kwa Muhammad Mubarak Salim , msimamizi mkuu wa posta Lamu island.
ENGLISH: Ustadh Mau is receiving a present by Muhmmad Mubarak Salim, post master of Lamu island.
SWAHILI: Ustadh Mau was invited to take part to a farewell celebration for Athras Mohammad Ali aliyekuwa mkurugenzi wa elimu Lamu island. Mzee aliyekaa upande wa kulia nyuma ya Ustadh Mau ni Abdalla Iskandar aliyekuwa ami yake Athrash na seremala maarufu sana Lamu island. Sherehe ya kumwaga Athras Mohammad Ali ilifanyiwa Lamu Fort Museum.
ENGLISH: Ustadh Mau alikuwa amealikwa kwa sherehe ya kumwaga Athrash Mohammad Ali who was education officer of Lamu island. The elderly man on the right-hand side behinf Ustadh Mau is Abdalla Iskandar the uncle of Atrash and a reknown wood carpenter in Lamu island. The farewell celebration took place at Lamu island Fort Museum.
SWAHILI: Sura hii inayopendeza ya Ustadh Mau ilipigwa kwenya duka lake la mkate. Ustadh Mau alianza kuvaa miwani alipokuwa miaka thalatini na tatu.
ENGLISH: This beautiful portrait of Ustadh Mau was taken at his bakery. Ustadh Mau started wearing glasses when he was thirty-three years old.
SWAHILI: Picha ya Ustadh Mau nyumbani kwake. Sehemu ya kichwa haionekani.
ENGLISH: Picture of Ustadh Mau taken at his place. Unfortuantely his front is cut.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunaona Ustadh Mau anazawadiwa na kamishna kwa kua na mchango bora katika jamii ya Lamu island.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen receiving a Badge of Honour from a government official for his contributions to the community of Lamu island.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunaona Ustadh Mau anazawadiwa na kamishna kwa kua na mchango bora katika jamii ya Lamu island.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen receiving a Badge of Honour from a government official for his contributions to the community of Lamu island.
SWAHILI: Katika picha hii tunamuona Ustadh Mau akiwa amesimama mbele ya bakery ya familia yake.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen standing in front of his family's bakery.
SWAHILI: Ustadh Mau yuko kwenye picha hii kwa boni, kabila ambalo limesauliwa. Ni waislamu ingawa hawajui sana kuhusu dini. Ustadh alikwenda kuwatembelea huko madrasani kwao. Picha inaonyesha alipowaletea wanafunzi wa madrasa zawadi kama vitabu kalamu na paramendi kwa kusoma. Wakati huo walikuwa jamaa ya elfu tatu , wanaishi kwenye vijiji vitano: Bargoni, Mangai, Dede wa rede, Mlimani, Basuba (baina Mokowe na Kiunga, Lamu island West). Siku hizi kuna operesheni inayoitwa Operation Boni Forest kupambana na al-Shabab ambao wanafikiriwa kwamba wako Boni Forest.
ENGLISH: Ustadh Mau is amid the Boni people, an ethnic group that has been forgotten. As he puts it, "they are Muslims but they do not know enough about Islam" . Ustadh Mau went to visit them at their madrasa. The picture shows him bringing to them books, pens and candies. Back then the Boni group counted 3000 people. Boni people live in five villages: Bargoni, Mangai, Dede wa rede, Mlimani, Basuba (between Mokowe and Kiunga, Lamu island West). Currently an operation called Operation Boni Forest against al-Shabab is on.
SWAHILI: Katika picha hii Ustadh Mau anaonekana akizungumzisha kundi la watu katika eneo la Mkunguni, iliyoko katikati ya mji wa Lamu island. Mkutano huu uliandaliwa juu ya kuelimisha watu kuhusu afya na chanjo, ili kujenga watu imani ju ya umuhimu wa afya. Mmoja wa wa aliyesimama nyuma ya ustadh ni afisa wa afya.
ENGLISH: On this picture Ustadh Mau is seen speaking to a crowd on Mkunguni, Lamu island's town square. The gathering was held to raise awareness on health issues and vaccines, in order to motivate people to take care of one's own and eachother's health. The man behind Ustadh was a health officer.