SWAHILI: Ustadh Mau yuko kwenye picha hii kwa boni, kabila ambalo limesauliwa. Ni waislamu ingawa hawajui sana kuhusu dini. Ustadh alikwenda kuwatembelea huko madrasani kwao. Picha inaonyesha alipowaletea wanafunzi wa madrasa zawadi kama vitabu kalamu na paramendi kwa kusoma. Wakati huo walikuwa jamaa ya elfu tatu , wanaishi kwenye vijiji vitano: Bargoni, Mangai, Dede wa rede, Mlimani, Basuba (baina Mokowe na Kiunga, Lamu island West). Siku hizi kuna operesheni inayoitwa Operation Boni Forest kupambana na al-Shabab ambao wanafikiriwa kwamba wako Boni Forest.
ENGLISH: Ustadh Mau is amid the Boni people, an ethnic group that has been forgotten. As he puts it, "they are Muslims but they do not know enough about Islam" . Ustadh Mau went to visit them at their madrasa. The picture shows him bringing to them books, pens and candies. Back then the Boni group counted 3000 people. Boni people live in five villages: Bargoni, Mangai, Dede wa rede, Mlimani, Basuba (between Mokowe and Kiunga, Lamu island West). Currently an operation called Operation Boni Forest against al-Shabab is on.
SWAHILI: Katika picha hii tunamuona Ustadh Mau akiwa amesimama mbele ya bakery ya familia yake.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen standing in front of his family's bakery.
SWAHILI: Ustadh Mau anaonekana kwenye mkusanyiko wa watu katika eneo la shanga ndani ya kisiwa cha Pate. Ustadh alialikwa kueka jiwe la msingi kwa minajili ya kujengwa mskiti mpya.
ENGLISH: Ustadh Mau is depicted at a gathering in Shanga, a village on Pate islandIsland. Ustadh was invited to lay down the foundation stone (jiwe la msingi) for a new mosque there.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunamuona Ustadh Mau akisoma Texas Review alichozawadiwa na jirani yake kutoka Uamerika akiwa nje ya nyumba yake.
ENGLISH: In this picture Ustadh is reading the Texas Review given to him by his American neighbour. Ustadh was standing outside of his house in the picture.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunaona Ustadh Mau anazawadiwa na kamishna kwa kua na mchango bora katika jamii ya Lamu island.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen receiving a Badge of Honour from a government official for his contributions to the community of Lamu island.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunaona Ustadh Mau anazawadiwa na kamishna kwa kua na mchango bora katika jamii ya Lamu island.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen receiving a Badge of Honour from a government official for his contributions to the community of Lamu island.
SWAHILI: Katika picha hii Ustadh Mau anaonekana akizungumzisha kundi la watu katika eneo la Mkunguni, iliyoko katikati ya mji wa Lamu island. Mkutano huu uliandaliwa juu ya kuelimisha watu kuhusu afya na chanjo, ili kujenga watu imani ju ya umuhimu wa afya. Mmoja wa wa aliyesimama nyuma ya ustadh ni afisa wa afya.
ENGLISH: On this picture Ustadh Mau is seen speaking to a crowd on Mkunguni, Lamu island's town square. The gathering was held to raise awareness on health issues and vaccines, in order to motivate people to take care of one's own and eachother's health. The man behind Ustadh was a health officer.
SWAHILI: Ustadh Mau anapokea zawadi kutoka kwa Muhammad Mubarak Salim , msimamizi mkuu wa posta Lamu island.
ENGLISH: Ustadh Mau is receiving a present by Muhmmad Mubarak Salim, post master of Lamu island.
SWAHILI: Sura hii inayopendeza ya Ustadh Mau ilipigwa kwenya duka lake la mkate. Ustadh Mau alianza kuvaa miwani alipokuwa miaka thalatini na tatu.
ENGLISH: This beautiful portrait of Ustadh Mau was taken at his bakery. Ustadh Mau started wearing glasses when he was thirty-three years old.
SWAHILI: Picha ya Ustadh Mau nyumbani kwake. Sehemu ya kichwa haionekani.
ENGLISH: Picture of Ustadh Mau taken at his place. Unfortuantely his front is cut.
SWAHILI: Ustadh Mau was invited to take part to a farewell celebration for Athras Mohammad Ali aliyekuwa mkurugenzi wa elimu Lamu island. Mzee aliyekaa upande wa kulia nyuma ya Ustadh Mau ni Abdalla Iskandar aliyekuwa ami yake Athrash na seremala maarufu sana Lamu island. Sherehe ya kumwaga Athras Mohammad Ali ilifanyiwa Lamu Fort Museum.
ENGLISH: Ustadh Mau alikuwa amealikwa kwa sherehe ya kumwaga Athrash Mohammad Ali who was education officer of Lamu island. The elderly man on the right-hand side behinf Ustadh Mau is Abdalla Iskandar the uncle of Atrash and a reknown wood carpenter in Lamu island. The farewell celebration took place at Lamu island Fort Museum.
SWAHILI: Huyu ni shangazi wa Ustadh Mau anayeitwa Rabia Abdulkadir, dada wa babake Ustadh Mau Ahmad Abdulkadir. Alipozaliwa Ustadh Mau shangazi alikuwa ameshafariki. Dada moja mkbubwa wa Ustadh Mau aliitwa kama shangazi yake Rabia. Wadada wengine waliitwa Nuru, Sophia na Amina. Picha inawezekana ilikuwa imepigwa Mombasa baada shangazi Rabia aliolewa.
ENGLISH: This is Ustadh Mau's aunt called Rabia Abdulkadir, sister of Ahmad Abdulkadir who was born in Lamu island. She already passed away when Ustadh Mau was born. One of Ustadh Mau's sister was called Rabia like their aunt. Ustadh Mau's other sisters are called Nuru, Sophia and Amina. This picture was likely taken in Mombasa after that aunt Rabia got married.
SWAHILI: Ustadh Mau anasimama karibu na rasa za maktaba yake. Hii ni sehemu ya kwanza aliyoitengeneza nyumbani Langoni kabla alipojenga ghorofa nyingine kubwa zaidi baadaye. Vitabu vinavyoonyeshwa ni vitabu vya dini khususan kwa kiarabu na baadhi kwa kingereza.
ENGLISH: Ustadh Mau is standing close to his book shelves. This is the beginning of his library that he put on in Langoni, before building a seprate bigger room on the second floor for it later on. The books shown are mainly Arabic books and a few in English.
SWAHILI: Hii ni picha ya madrasa ya kitambo mjini Lamu island aliposomea Ustadh Mau. Madrasa hii ilikua ya pili kuanzishwa Kenya nzima. Jumba la madrasa hiyo limeporomoka na kuwa gofu sahii.
ENGLISH: This is a photograph of an old madrasa in Lamu island. This was the second madrasa to ever open in Kenya. Later, the building collapsed and got destroyed.
SWAHILI: Picha hii inarejelea msaada wa watu wa Matondoni walipoingiliwa na moto. Lamu island Muslim Youth alileta cimiti na milango. Mtu anayesimama upande wa kulia wa Ustadh Mau anaitwa Karim Rajan aliyekuwa mwanahabari wa gazeti la 'Nation'. Mtu aliyesimama mbali mwenye kanzu nyeupe karibu na mifuko ya cimiti ni mmoja wa mwanchama - kama vile vile Ustadh Mau - wa Lamu island Muslim Youth.
ENGLISH: This photo goes back to the help provided to the people of Matondoni during a fire. Lau Muslim Youth carries cement and doors. The person who stands on the right-hand side of Ustadh Mau is called karim Rajan who was the reporter for the Nation newspaper. The person on the back wearing the white gown (kanzu) close by the bags of cement – like Ustadh Mau – was one of the member of Lamu island Muslim Youth.
SWAHILI: Wakati wa ukosefu wa ngano nchi nzima Kenya, Ustadh Mau hakuweza kuendelea kufanya kazi dukani kwake la mkate na ndio maana kwa muda alianza kushughulika sokoni kama muuzaji wa nyama. Ustadh alikuwa na miaka 28 takriban kwenye picha.
ENGLISH: During the caresty of wheat in the whole country of Kenya, Ustadh Mau could not work at his bakery and this is why he started for a while to work at the market as seller of meat. Ustadh Mau was around 28 years old.