SWAHILI: Ustadh Mau yuko kwenye picha hii kwa boni, kabila ambalo limesauliwa. Ni waislamu ingawa hawajui sana kuhusu dini. Ustadh alikwenda kuwatembelea huko madrasani kwao. Picha inaonyesha alipowaletea wanafunzi wa madrasa zawadi kama vitabu kalamu na paramendi kwa kusoma. Wakati huo walikuwa jamaa ya elfu tatu , wanaishi kwenye vijiji vitano: Bargoni, Mangai, Dede wa rede, Mlimani, Basuba (baina Mokowe na Kiunga, Lamu island West). Siku hizi kuna operesheni inayoitwa Operation Boni Forest kupambana na al-Shabab ambao wanafikiriwa kwamba wako Boni Forest.
ENGLISH: Ustadh Mau is amid the Boni people, an ethnic group that has been forgotten. As he puts it, "they are Muslims but they do not know enough about Islam" . Ustadh Mau went to visit them at their madrasa. The picture shows him bringing to them books, pens and candies. Back then the Boni group counted 3000 people. Boni people live in five villages: Bargoni, Mangai, Dede wa rede, Mlimani, Basuba (between Mokowe and Kiunga, Lamu island West). Currently an operation called Operation Boni Forest against al-Shabab is on.
African American church wedding with the bride and groom beneath a canopy in the center and approximately 20 guests in the pews. Flowers adorn the church.
Grafton Tyler Brown was an African American who artist worked as a lithographer, cartographer and landscape painter capturing images of landscapes in the northwest United States, and British Columbia.
SWAHILI: Katika picha hii tunamuona Ustadh Mau akiwa amesimama mbele ya bakery ya familia yake.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen standing in front of his family's bakery.
SWAHILI: Ustadh Mau anaonekana kwenye mkusanyiko wa watu katika eneo la shanga ndani ya kisiwa cha Pate. Ustadh alialikwa kueka jiwe la msingi kwa minajili ya kujengwa mskiti mpya.
ENGLISH: Ustadh Mau is depicted at a gathering in Shanga, a village on Pate islandIsland. Ustadh was invited to lay down the foundation stone (jiwe la msingi) for a new mosque there.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunamuona Ustadh Mau akisoma Texas Review alichozawadiwa na jirani yake kutoka Uamerika akiwa nje ya nyumba yake.
ENGLISH: In this picture Ustadh is reading the Texas Review given to him by his American neighbour. Ustadh was standing outside of his house in the picture.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunaona Ustadh Mau anazawadiwa na kamishna kwa kua na mchango bora katika jamii ya Lamu island.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen receiving a Badge of Honour from a government official for his contributions to the community of Lamu island.
SWAHILI: Kwenye picha hii tunaona Ustadh Mau anazawadiwa na kamishna kwa kua na mchango bora katika jamii ya Lamu island.
ENGLISH: In this picture Ustadh is seen receiving a Badge of Honour from a government official for his contributions to the community of Lamu island.
SWAHILI: Katika picha hii Ustadh Mau anaonekana akizungumzisha kundi la watu katika eneo la Mkunguni, iliyoko katikati ya mji wa Lamu island. Mkutano huu uliandaliwa juu ya kuelimisha watu kuhusu afya na chanjo, ili kujenga watu imani ju ya umuhimu wa afya. Mmoja wa wa aliyesimama nyuma ya ustadh ni afisa wa afya.
ENGLISH: On this picture Ustadh Mau is seen speaking to a crowd on Mkunguni, Lamu island's town square. The gathering was held to raise awareness on health issues and vaccines, in order to motivate people to take care of one's own and eachother's health. The man behind Ustadh was a health officer.