SWAHILI: Picha ni kutoka warsha kuhusu UKIMWI mjini Mombasa. Mtu anayekaa karibu na Mahmoud Mau ni mtu kutoka Tana River. Viongozi vya dini wengi walikuwa wamealikwa.
ENGLISH: This picture was taken during a workshop on HIV held in Mombasa and organised by RISSEA ("Research Institute of Swahili Studies of Eastern Africa"). The person sitting close to Ustadh Mau is from Tana River. Many religious scholars took part at this meeting.
SWAHILI: Ustadh Mau anonegea nyumbani kwa mtu fulani lakini hakumbuki sana ilikuwa wapi na nani. Bila ya shaka wale ambao wanaketi walikuwa si Waislamu.
ENGLISH: Ustadh was talking at someone's place. The people sitting in the picture are not Muslim. He has vague memories of the exact context.
SWAHILI: Picha hii ilipigwa mwanzoni mwa mwaka wa elfu moja mia tisa na tisaini, katika kijiji kidogo kiitwacho Boni, katika maeneo ya Lamu island. Picha hii inaonesha Ustadh akipeana chakula na madaftri ya kidini kwa watoto kijijini wenye kuishi katika hali duni. Nyuma ya hii picha jina la ustadh likeandikwa kwa herufi za Kiarabu na pia ikieleza kwamba hii picha ilipgwa siku ya kwanza ustadh kuwasili Boni.
ENGLISH: This picture was taken in the early 1990's in Boni, a remote village in Lamu island. It depicts Ustadh Mau handing out donations (food and religious books) to the children of the village who live in difficult circumstances. On the back of this particular photograph Ustadh's name is written in Arabic as well as the information that that photograph was taken on the day of his arrival in Boni.
SWAHILI: Picha hii ilipigwa mwanzoni mwa mwaka wa elfu moja mia tisa na tisaini, katika kijiji kidogo kiitwacho Boni katika maeneo ya Lamu island. Picha hii inaonesha ustadh akipeana chakula na madaftari ya kidini kwa watoto wa kijijini wenye kuishi katika hali duni.
ENGLISH: This picture was taken in the early 1990's in Boni, a remote village in Lamu island. It depicts Ustadh Mau handing out donations (food and religious books) to the children of the village who live in difficult circumstances.
SWAHILI: Kwenye picha hii Ustadh Mau yuko katika duka la mkate ambalo ami yake alilinunua kutoka mhindi aliyeitwa Bachu, mtu wa madhehebu wa Ithnashari. Ustadh Mau amefanya kazi kwenye duka hilo la mkate kuanzia mwaka 1973 hadi 2005; baadaye alimwuzia mtoto wake wa kwanza anayeitwa Fatih. Mwaka 2015, Fatih alimwuzia kakake Yasseer (mtoto wa pili kwa upande wa mke wake wa kwanza) ambaye anashughulika nayo hadi siku hizi. Aina ya mkate kwenye picha ni madhura au "mascons" (kutoka Kingereza) na mikate mirefu yaani long rolls. Kipindi cha kula mkate ni kawaida jioni pamoja na chai na Blue Band.
ENGLISH: Ustadh Mau is here portrayed in the bakery that his uncle bought. The bakery was earlier run by an Indian man known as Bachu belonging to the Ithnashari school. Ustadh Mau has worked in the bakery from 1973 up to 2005, afterwards he passed it over and sold it to his first son Fatih. In 2015, Fatih sold it to his brother and up to nowadays the bakery his run by Yasser, Ustadh Mau's second born (from his first wife). The bread in the picture is known as scons (from English) and long rolls. The preferred time to consume bread until nowadays is in the evening, with tea and butter.
SWAHILI: Katika picha hii tunamuona Ustadh Mau akiwa na rafiki yake Abdallah Jumaan wakiogelea baharini.
ENGLISH: In this photograph Ustadh Mau and his friend Abdallah Jumaan are pictured, swimming together in the sea.
SWAHILI: Picha hii ilipigwa na jirani mzungu ( mume wake Madam Joss) wa Ustadh Mau mta mwini. Yalikuwa mazoea yao kukaa barazani nde ya nyumba yake kuongea na kunywa kahawa hadi magharibi. Wale ambao wanakaa kuanzia upande wa kushoto ni Abdalla Jumaani, Bwana Omar, Abdalla Quresh, Mahsen Alwi na Ustadh Mau. Wazee wote wameshafariki.
ENGLISH: This picture was taken by the husband of Miss Joss who offered to the baraza some coffee. They used to meet there every afternoon to chat and have coffee until sunset. The people sitting are (starting from the left-hand side): Abdalla Jumaani, Bwana Omar, Abdala Quresh, Mahsen Alwi and Ustadh Mau. All Ustadh Mau's friends have already passed away.
SWAHILI: Picha hii ilipigwa mwanzoni mwa mwaka wa elfu moja mia tisa na tisaini, katika kijiji kidogo kiitwacho Boni katika maeneo ya Lamu island. Picha hii inaonesha Ustadh akipeana chakula na madaftari ya kidini kwa watoto wa kijijini wenye kuishi katika hali duni.
ENGLISH: This picture was taken in the early 1990's in Boni, a remote village in Lamu island. It depicts Ustadh Mau handing out donations (food and religious books) to the children of the village who live in difficult circumstances.
Poster depicts an illustration of the Virgin Mary holding Jesus as a Child with four archangels looking down upon them; the Virgin Mary is wearing a blue hooded robe with yellow tassels, sunbursts, and stars; Jesus is wearing a red robe and holding a book; behind the Virgin Mary and Jesus is a red background with a yellow floral pattern; three of the archangels appear to hold swords; at the top is a border composed of red leaves and blue flowers.