SWAHILI: Ustadh Mau anaonekana kwenye mkusanyiko wa watu katika eneo la shanga ndani ya kisiwa cha Pate. Ustadh alialikwa kueka jiwe la msingi kwa minajili ya kujengwa mskiti mpya.<br>ENGLISH: Ustadh Mau is depicted at a gathering in Shanga, a village on Pate islandIsland. Ustadh was invited to lay down the foundation stone (jiwe la msingi) for a new mosque there.
SWAHILI: Ustadh Mau anasimama karibu na rasa za maktaba yake. Hii ni sehemu ya kwanza aliyoitengeneza nyumbani Langoni kabla alipojenga ghorofa nyingine kubwa zaidi baadaye. Vitabu vinavyoonyeshwa ni vitabu vya dini khususan kwa kiarabu na baadhi kwa kingereza.<br>ENGLISH: Ustadh Mau is standing close to his book shelves. This is the beginning of his library that he put on in Langoni, before building a seprate bigger room on the second floor for it later on. The books shown are mainly Arabic books and a few in English.